Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa amefanya ukaguzi wa kituo cha Afya na Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 13 katika shule ya Sekondari Majimoto Vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.
Akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Amesema Serikali ya Awamu ya sita inalenga kuwatumikia wananchi inaleta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wananchi hivyo haitavumilia kuona Watumishi wakileta uzembe katika kusimamia miradi inayoendelea kwa ukamilifu au kula fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya maendeleo.
Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Watumishi wawe na utaratibu wa kutembelea wananchi katika vijiji ikiwa katika siku sita za Juma sikutatu ziwe za kutembelea Wananchi.
Waziri Mkuu amefurahishwa na kasi na usimmizi mzuri wa ujenzi wa Mradi wa kituo cha Afya Ikulwe na Ujenzi wa Vyumba vya madarasa 13 shule ya sekondari Majimoto ambao unaendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Aidha amemuagiza Mkurungenzi Mtendaji kuhakikisha vifaa vinakamilika katika kituo cha Afya cha Ikulwe ili kituo hicho kianze kufanya kazi tarehe 27 /12/2022 ili wananchi waweze kupata huduma kutokana na kuikosa kwa muda mrefu .
Awali akisoma Taarifa ya kituo cha Afya Ikulwe Mkurungenzi Mtendaji Bi. Catherine Mashalla amesema kituo hiki cha Afya kitaweza kuhudumia idadi kubwa ya wananchi katika Kata ya Majimoto na vitongoji vyake ambapo itasaidia kupunguza idadi ya msongamano wa wagonjwa katika zahanati na vifo vya wakina mama wajawazito .
Pia amesema ujenzi huu wa kituo cha Afya Ikulwe kwa mujibu wa mkataba unatarajiwa kukamilika ifikapo 20/2/2023 ikiwa umekamilisha Ujenzi wa jengo la wangonjwa wanje, Ujenzi wa jengo la mama na mtoto, Ujenzi wajengo la upasuaji, ujenzi wa jengo la maabala ,ujenzi jengo la kufulia na vyoo vya nje 7 ambapo ujenzi huu utagalimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 423,890,000.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa