Kamati hii ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe imekagua , Ukamilishaji wa ofisi ya Mtendaji wa kata Ikuba , Ujenzi wa shule Mpya ya Sekondari Ikuba na Ujenzi wa Maabara Shule ya Sekondari Chamalendi.
Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mhe. Silas Ilumba amepongeza kwa ukamilishaji wa jengo la Ofisi ya Mtendaji wa Kata kwani kukamilika kwa jengo hilo kutarahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mwenyekiti pamoja wanakamati wameshauri kupanda miti katika eneo la ofisi kwa kuwa upandaji wa miti unafaida nyingi ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ilitoa fedha kiasi cha Tsh 9,600,000 kwa ajili ya ujenzi huo ambapo Ujenzi umetumia kiasi cha Tsh. 9,336,950 mpaka kukamilika.
Katika ziara hiyo wamepongeza juu ya ujenzi wa Shule ya mpya ya Sekondari Ikuba ambayo ujenzi wake una kwenda kwa kasi na wakuvutia zaidi kutokana usimamizi mzuri uliopo.
Kamati hii imeridhika na ujenzi huo wa shule mpya ambapo Serikali ilitoa fedha kiasi cha Tsh. 603,890,562 kwa ajili ya kuwapunguzia wanafunzi kuweza kuepuka kutembea umbali mrefu .
Aidha wametembelea Maabara tatu za shule ya Sekondari Chamalendi ambapo wamemwagiza mkaguzi wandani kufatilia ilikuweza kujiridhisha na matumizi ya fedha ambayo yametumika kwani maabara hizo hazijajengwa kwa viwango vinavyo takiwa.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa